Klabu ya Liverpool imeonyesha ni tofauti na huku kwetu baada ya kumshitaki mshambuliaji wake, Mohamed Salah baada ya kuonekana akiendesha gari huku akichati na simu.
Salah alirekodiwa na baadhi ya mashabiki wa Liverpool akiwa kwenye foleni, baadhi ya mashabiki hao walitaka kuzungumza naye, lakini hakufungua kioo.
Taratibu aliendelea kuchati huku akisogea taratibu na baada ya video hiyo kuzagaa mitandaoni, Liverpool ikaripoti polisi kwa tabia hiyo ya Salah kuendesha huku anatumia simu.
Tayari imeelezwa, Jeshi la Polisi jijini Liverpool, limeanza kulifanyia uchunguzi suala hilo.
0 COMMENTS:
Post a Comment