AMUNIKE AWAITA 30 STARS KWA AJILI YA KUWAVAA CAPE VERDE, SIMBA PIA WAMO
Na George Mganga
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Emmanuel Amunike, ametangaza kikosi cha wachezaji 30 watakoacheza mechi ya kufuzu AFCON 2019 dhidi ya Cape Verde Oktoba 12 2018
Magolikipa
1. Aishi Manula (Simba)
2. Mohamed Abdulrahman (JKT)
3. Benno Kakolanya (Yanga)
Mabeki
4. Shomary Kapombe (Simba)
5. Hassan Kessy (Nkana, Zambia)
6. Salum Kimenya (Tz Prisons)
7. Gadiel Michael (Yanga)
8. Paulo Ngalema (Lipuli)
9. Ally Sonso (Lipuli)
10. Kelvin Yondani (Yanga)
11. Abdi Banda (Baroka, Afrika Kusini)
12. Abdallah Kheri (Azam)
13. Agrey Morris (Azam)
14. Andrew Vincent Dante (Yanga)
15. David Mwantika (Azam)
Viungo
16. Himid Mao (Pertojet, Misri)
17. Jonas Mkude (Simba)
18. Mudathir Yahya (Azam)
19. Feisal Salum (Yanga)
20. Frank Domayo (Azam)
21. Saimon Msuva (El Jadidi, Morocco)
22. Farid Mussa (CD Tenerife, Hispania)
23. Salum Kihimbwa (Mtibwa)
Washambuliaji
24. Mbwana Samata (Genk, Ubelgiji)
25. John Bocco (Simba)
26. Thomas Ulimwengu (A Hilal, Sudani)
27. Rashid Mandawa (BDF XI, Botswana)
28. Yahya Zayd (Azam)
29. Shaban Chilunda (CD Tenerife, Hispania)
30. Kelvin Sabato (Mtibwa Sugar)
Wapi Ibrahim Ajibu, Kichuya na Nyoni.
ReplyDeleteHata ajibu hayupo duh na kichuya kweli zama zimebadilika
ReplyDeletehuyu coach anajua tazama selection yake kaleta wacheza 9 toka nje ambao ni prossional players na kachukua wachezaji 21 toka timu saba (7) zinazocheza ligi kuu !! makocha wetu wangetujazia wachezaji wa Simba na Yanga tu lakini kachukua 6 toka azam na 5 yanga na 4 toka Simba Jkt mmoja Lipuli wawili Prison mmoja na Mtibwa wawili - very good combination
ReplyDeleteCombination nzuri ya timu haichaguliwi kwa mfumo wa kisiasa kwamba eti kila timu lazima itoe mchezaji au kwa idadi ya wachezaji sawa bali kwa ubora wa uchezaji. Kocha mzuri awezi hata kidogo akamuacha Ibrahim Ajib akiwa katika ubora huu na kumchukua Ally Sonso ambaye bado mchango wake huko Lipuli sio hata nusu ya mchango aliotoa SALAMBA. Ajabu sana. Anawezaje kumuacha Erasto Nyoni akiwa katika ubora wake na kumchukua Abdallah Kheri wa Azam ambaye hata Azam kwenyewe hayuko first eleven? Kwa Kichuya sitaki kumuongelea maana kila mmoja anajua kazi na umuhimu wake katika timu ya taifa. Kumbuka mechi yake ya mwisho stars dhidi ya DRC iliyokuwa imesheheni wa kulipwa. Kocha wa DRC aliuliza kama Kichuya ni wa kimataifa maana aliupiga mwingi na hata kwenye klabu yake ni chagua la kwanza.
ReplyDeleteKocha anaangalia fitness ya mchezaji dk 90, na uwezo wake wa kukaba akipokonywa mpira, Migomba ana kipaji ila pumzi inawahi kata na uwezo wake wa kunyang'anya mipira ni mdogo
ReplyDeleteKOCHA TUAMBIE LEO HII WACHEZAJI WAENDE KAMBINI WAPI MZEE TUSIRUDIE UTOVU WA NIDHAMU TIMU YA TAIFA KWANZA VILABU BAADAE SANA. KURIPOTI LEO SAA NGAPI MWISHO?
ReplyDeleteKocha umefanya makosa kumuacha kichuya kwani ilibidi winga sumbugu namba 7 Msuva namba 11 Kichuya hapo ingepende xana
ReplyDeleteTukisema mtarudishia ya usimba na uyanga lakini ukweli tupu huo wanaousema wengine - KICHUYA, AJIBU, ERASTO NYONI.
ReplyDeleteAjibu, Nyoni????????????
ReplyDeleteKimsimgi kuna wachezaji wameitwa ili kukamilisha idadi lakini sio kuleta ushindani wa namba ndani ya stars. Kuwaacha wachezaji wa Simba na Yanga kwa sababu ya kuepuka usimba na uyanga japo kuwa wanauwezo huo ni ujinga.Waganda licha ya Juuko kutoichezea timu yake kwa kipindi lakini hawakuawacha kumuita cha msingi ukiacha wachezaji wanaocheza nje ni timu tatu nchini Azam,Yanga na Simba ndio timu zenye wachezji amabo wanauzoefu na mechi za kimataifa na wameshasafiri nchi kadhaa na wameshapata changamoto za makocha kadhaa wa kigeni wenye uzoefu kwa hivyo kupanga ni kuchagua kila la kheri stars.
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeletekocha kama umeshindwa bara usema sisi tunataka ushindi na si maneno.
ReplyDelete