September 27, 2018


Kocha Mkuu Emmanuel Amunike leo majira ya saa 5 atakitangaza kikosi cha Taifa Stars kitakachoweka kambi maalum hivi karibuni tayari kwa maandalizi ya kusaka tiketi ya AFCON 2019 dhidi ya Cape Verde.

Stars itakuwa na kibarua ugenini dhidi ya Cape Verde mchezo ambao utapigwa Oktoba 12 kusaka tiketi ya kufuzu AFCON.

Ikumbukwe Kocha huyo aliwaondoa wachezaji 6 wa Simba mara ya mwisho baada ya kuwaita kuelekea mechi dhidi ya Uganda iliyopigwa jijini Kampala.

Baada ya kutangazwa kwa wachezaji leo, Stars itaanza kambi siku chache zijazo kujiandaa na kipute hicho tayari kukabiliana na Verde tarehe tajwa hapo juu.

1 COMMENTS:

  1. hao wachezaji sijui anawaona saa ngapi wakati hafatilii mechi za ligi kuu maana baada ya mechi na Uganda alisepa kurudi kwenye familia yake Hispania

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic