September 17, 2018


Mlinda Mlango mlango wa klabau ya Yanga, Beno Kalonya, ameivbuka na kufunguka kwa kile alichokieleza Kocha wake Mkuu, Mwinyi Zahera jana kuwa hakumchezesha kwa kuwa alifanya mazoezi siku moja pekee, imeelezwa.

Zahera alisema kuwa Kakolanya aliamua kumuweka benchi mchezaji huyo kutokana na kuamini kuwa hakuwa fiti kiasi cha kwamba akashindwa kumpanga.

Baada ya Zahera kueleza hayo jana, Kakolanya ameibuka akisema ameshangazwa na kauli hiyo akisema alijumuika na timu kwenye mazoezi tangu kikosi hicho kilipoingia wiki jana kujiandaa na mechi dhidi ya Stand.

Kipa huyo ameeleza kuwa Zahera aliamua kueleza hayo labda alikuwa na sababu zake za msinfi lakini akisema si kweli kuwa alifanya mazoezi kwa siku moja pekee.

Katika mechi dhidi ya Stand United ambayo Yanga iliibuka na ushindi wambao 4-3, Kalolanya alikuwa kwenye kikosi cha akiba ambapo hakuweza kucheza dakika zote 90.

Zahera alimuweka kipa Mkongo Klaus Kindoki langoni ambaye aliibua lawama na malalamiko kutokana na kufungwa mabao matatu kiulaini na mashabiki wa timu hiyo kuutaka uongozi kumuweka benchi ili ajifunze.




6 COMMENTS:

  1. Jamani tusianze vurugu za kumuingilit kocha kwenye kupanga kikosi. Hiyo ni kazi ya kocha na benchi la ufundi kwanini mnataka kuanza vurugu?

    ReplyDelete
  2. KOCHA ANA UCHUNGU SANA NA YANGA. TUSIMVURUGE. AMESEMA ATAONGEA NA TIMU ZA TP MAZEMBE NA VITA A.S ILI KILA MWAKA WACHEZAJI WAWILI WA YANGA WACHEZE KWENYE VILABU HIVYO VYA DRC.

    ReplyDelete
  3. Pamoja na mapenzi kwa Kocha Zahera lakin kwa hili la jana kachemka mara mbili, kwanza kwa kumpanga Kipa Kindoki kucheza na beki iliyokuwa na mapungufu akiwa hajaozoea sana; kipa huyu ni mzito, pili kwa matamshi yake juu ya Beno; kama Mkuu wa benchi la ufundi hakutakiwa kusema yote hayo, ukubwa dawa huwa tunabakisha kocha.
    Nimalizie tu huyu kipa Kindoki bado saana

    ReplyDelete
  4. kwa hiyo kama atawapeleka KONGO Hao wachezaji ndo aboronge then watu wakae kimya?

    ReplyDelete
  5. Kocha anauchungu na yanga kutuzidi wanayanga? Akizngua atasepa tu

    ReplyDelete
  6. Kocha anauchungu na yanga kutuzidi wanayanga? Akizngua atasepa tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic