September 7, 2018


Kuelekea mechi ya kuwania kufuzu AFCON 2019 kati ya Uganda dhidi ya Taifa Stars, beki katili wa The Cranes, Juuko Murushid ameahidi kumuweka kati Mbwana Samatta.

Licha ya kuonesha kiwango cha juu akiwa na klabu yake ya KRC Genk huko Ubelgiji, Murushid ameahidi kumzuia vizuri Samatta asiweze kuleta msala mbele yao kwa kuhakikisha hapiti eneo la ulinzi.

Beki huyo ambaye bado ana mkataba na Simba kwa mujibu wa uongozi wa klabu, ana imani watapata matokeo dhidi ya Stars kutokana na kuwa na kikosi kizuri chenye wachezaji wengi wanaocheza nje ya taifa lao.

Aidha, Murushid ametamba kuwa amecheza dhidi ya washambuliaji walio bora zaidi ya Samatta hivyo haoni tabu kumalizana naye kirahisi kwenye Uwanja wao wa nyumbani.

Uganda inaenda kucheza na Stars ikiwa na kumbukumbu ya kuwafunga Cape Verde bao 1-0 kwenye mechi ya kwanza ya kundi L wakati Stars ikibanwa mbavu kwa matokeo ya 1-1 na Lesotho jijini Dar es Salaam.

5 COMMENTS:

  1. Bado huwa nawashangaa sana Simba kuhusiana na Juuko Murshidi. Na kama Juuko atapata nafasi ya kucheza mechi na Stars weekend hii basi kunauwezekano mkubwa hata kocha wao wa sasa wa Simba akawashamgaa viongozi wake. Simba inajiandaa kuleta upinzani wa kweli kwenye mashindano ya Africa halafu utamuachaje mchezaji mwenye uzoefu kama Juuko?

    ReplyDelete
    Replies
    1. hata mimi nawashangaa unawezaje kumwacha mchezaji ambaye anachezea timu ya taifa ambayo ipo katika kiwango cha juu, pamoja na kujitapa juu ya uwekezaji bado pale mambo yanaenda kienyeji

      Delete
    2. usiangalie upande mmoja wa shillingi.Hivyo sidhani ni busara kuwalaumu viongozi.Pengine makubaliano kwenye mkataba hawajaafikianaa au mchezaji mwenyewe hapendi kuendelea kuchezea Simba.Nakumbuka pia benchi la ufundi chini ya Omog na Leachntre kuhusu report zao zilirecommend nini?

      Delete
  2. Hana uwezo wa kumzuia Samatta, labda kama atakuwa hajaamua kwa kuogopa kupata majeraha na wakati klabu yake inamuona lulu. Samatta ni habari nyingine bwana, achana nae kabisa. Amuulize pande la mtu Yaya Toure na yule beki wa Bukina faso aliyepigwa chenga mpaka akakaa chini. Labda asiamue kucheza kwa kiwngo cha kushindana.

    ReplyDelete
  3. Juurko Murshid hajasema maneno hayo. Ni Mwandishi ametafuta kiki ya kutawanya habari

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic