September 17, 2018


Na George Mganga

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemtangaza rasmi straika wa klabu ya Simba, Meddie Kagere kuwa mchezaji bora wa mwezi Agosti katika Ligi Kuu Bara.

Kagere amekuwa mchezaji wa kwanza katika msimu huu wa 2018/19 kushinda tuzo hiyo ambayo hutolewa kila baada ya mwezi mmoja.

Straika huyo ameisaidia Simba kuibuka na alama 6 za Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons na Mbeya City huku akifunga mabao matatu.

Kagere 'MK14' ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda Joseph Mahundi wa Azam na Omary Mponda wa Kagera Sugar walioingia tatu bora katika kuwania Tuzo hiyo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic