September 3, 2018


Mara baada ya kibali chake kupatikana, kiungo mchezeshaji wa Simba ambaye ni raia wa Zambia, Clatous Chama amesisitiza kwamba anakuja na moto wa hatari.

Chama alishindwa kuichezea Simba kwenye michezo yake miwili ya mwanzo wa ligi kutokana na klabu yake ya Power Dynamos aliyokuwa anaichezea kabla ya kutua Simba kushindwa kutuma ITC yake kwa wakati. Alikosa michezo ya Simba dhidi ya Prisons na Mbeya City.

Kwa mujibu wa Spoti Xtra, kiungo huyo ambaye kwa sasa ameitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Zambia ‘Chipolopolo’ amefunguka na kuelezea namna anavyokuja kitofauti. 

Kila kitu kimeenda sawa na nitaanza kucheza hivi karibuni. Kwangu ni jambo zuri kwani nitaanza majukumu katika klabu yangu mpya, niseme tu wazi nitapambana kuona klabu yangu inafanya vizuri kwenye mechi zake, wengi wasubiri kuona ni nini ambacho nitafanya kwa ajili ya timu.

Kutokana na ujio wake ndani ya Simba, kuliibuka mjadala mkubwa katika nafasi yake na Mnyarwanda, Haruna Niyonzima kuwa ana uwezekano wa kuchukua nafasi kwa asilimia 100.

Jambo lilipelekea Niyonzima kusema kuwa hastahili kulinganishwa na Chama kutokana na makubwa aliyoyafanya kwenye ligi ya hapa Tanzania na pia akashauri si vema kulinganishwa naye sababu wote wanacheza klabu moja.

3 COMMENTS:

  1. Chama Chama Chama. Mchezaji bora kabisa wa kiwango cha juu

    ReplyDelete
  2. Kwanza anacheza Zambia national team so aheshimiwe

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic