September 5, 2018





Uongozi wa Yanga umekanusha baadhi ya viongozi wa timu yao kukamtwa ofisini kwao na kwenda kuhojiwa na Taasisi ya Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Hiyo, ikiwa saa chache kuwepo na taarifa za viongozi wa timu hiyo kukamatwa na taasisi hiyo  kwa ajili ya kwenda kuhojiwa ofisini kwao.

Akizungumza na SALEHJEMBE, Ofisa Habari wa timu hiyo, Dismas Ten alisema hizo taarifa za kukamatwa na viongozi wa timu hiyo na taasisi hiyo na kwenda kuhojiwa siyo ya ukweli.

Ten alisema, ukweli uliokuwepo ni Takukuru walifika kutembelea Makao Makuu ya timu hiyo yaliyokuwepo mitaa ya Twiga na Jangwani tangu wiki iliyopita kama wanapokwenda kwenye taasisi nyingine na siyo kwa ubaya.

“Tumeshangazwa na uvumi unaondelea kwenye mitandao kuhusiana na taarifa za viongozi wa Yanga kukamatwa na Takukuru kwa ajili ya kwenda kuhojiwa kitu ambacho siyo sahihi.

“Maafisa hao wa Takukururu hawakufika siku mbili hizi kama inavyoelezwa, walifika tangu wiki iliyopita na walikuja kutembea kama wanavyokwenda kutembelea taasisi nyingine,”alisema Ten.

1 COMMENTS:

  1. Kawaida yetu Watanzania tulio wengi ni kufuata mkumbo na kushabikia fununu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic