September 5, 2018


Timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars" inayodhaminiwa na bia ya Serengeti Premium Lager inatarajia kuondoka Kesho Alhamis Septemba 6,2018 saa 7 mchana kuelekea nchini Uganda kwa mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza Afcon dhidi ya Uganda. 

Tutaondoka na kikosi cha wachezaji 23 na viongozi 7 watakaoambatana na viongozi mbalimbali wa TFF. 

Ni mchezo tunaokwenda kwa nia ya kufanya vizuri na kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kundi letu.

Kufanya vizuri kwa timu hii ni fahari ya kila Mtanzania tuendelee kuiunga mkono timu hii inayokwenda kupeperusha bendera ya Tanzania. 

Kocha Emmanuel Amunike anasema anaendelea na maandalizi akiendelea kuangalia mapungufu mbalimbali na kuyafanyia kazi ambapo anaamini kikosi kilichopo huku wachezaji wanaocheza nje wakiwa wameripoti wote. 

Anasema kikosi kina muelekeo mzuri na maelekezo anayotoa anaona yanaeleweka. 

Nahodha Mbwana Samatta amesema mchezo huo utakuwa wa ushindani na kikubwa ni kufuata matokeo mazuri kwenye mchezo huo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic