HAJI MANARA AUZUNGUMZIA MCHEZO WA YANGA NA STAND 'WALITAMANI MPIRA UISHE'
Ofisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, ameibuka na kuwapiga dongo watani zake wa jadi kuwa mpira waliocheza dhidi ya Stand United jana walitamani mechi iishe mapema.
Manara amefunguka na kueleza kuwa Yanga haikucheza mpira wa kifundi na badala yake walizidiwa kimbinu jambo ambalo lilisababisha wakoswe mabao kadhaa.
Ofisa Habari huyo mwenye maneno mengi zaidi, ameeleza kuwa Yanga waliona hali ngumu na kuanza kuomba mechi iishe haraka ili wasalie na matokeo yao ambapo walikuwa wanaongoza.
Mara baada ya Alex Kitenge kufunga bao la tatu, Manara aliamini kuwa Stand wangeweza kusawazisha na kuongeza mengine kutoka na watani zake walianza kuelemewa uwanjani.
Katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Taifa jana, Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-3 huku kipa wake Mkongo Klaus Kinzi Kindoki akipewa lawama juu ya mabao aliyofungwa.








MPIRA DAKIKA 90 ZITAPOISHIA NDIPO HAPO. YANGA WAMESHINDA GOLI 4 KWA 3. FOWADI INA UCHU WA MAGOLI. MANARA SIMBA INATAKIWA KUPATA MABAO. MPIRA MABAO , DROO HIZI ZILITUNYIMA UBINGWA MIAKA MICHACHE ILIYOPITA.
ReplyDeleteWe haji kwani ww ni msemajiYangYanga, basi rudi mtwara ukaendelee kuchezakucheza labda uushindi
ReplyDeletePoyoyooo unaacha kuzungumzia Simba, unakimbilia kusema mambo ya Yanga weye!
ReplyDeleteChizi huyo. Mbona haongelei habari ya Bigirimana Blaise alichowafanya Vibaka FC ligi iliyoisha hapohapo Taifa?
ReplyDelete