September 17, 2018


Baada ya Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Stand United ya Shinyanga kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee Yanga, Ibrahim Akilimali, amesema wanamuombea Beno Kakolanya apone haraka.

Akilimali amesema hajafurahishwa na kiwango cha kipa Mkongomani, Klaus Kindoki ambaye aliruhusu mabao matatu kiulaini na kusababisha kuondoa ladha ya ushindi walioupata.

Mzee huyo ambaye ni moja ya waasisi wa klabu ya Yanga, ameeleza kuwa Kindoki anapaswa kupewa muda baada ya kuonesha mapungufu jana na kusababisha kupigwa bao tatu na wapiga debe wa Shinyanga.

Aidha, Akilimali amewataka wanayanga kumwombea haraka kipa wao Beno Kakolanya maana ndiye anayemuani kuwa ataokoa jahazi ndani ya Yanga.

Beno amekuwa majeruhi kwa muda jambo ambalo lilipelekea kutocheza mechi hiyo japo alikuwa katika kikosi cha akiba.

Ukiachana na Kakolanya, Akilimali pia amesema amesikitishwa na washauri wa Kocha wao, Mwinyi Zahera baada ya kuwafanyia mabadiliko Ibrahim Ajibu na Mrisho Ngassa, akiamini kuwa walikuwa nguzi kuu.

Baada ya kutolewa kwa wachezaji hao Akilimali amesema Yanga ilipoteza kabisa nguvu na kuanza kuhaha huku Stand wakija juu.

Katibu huyo amewataka benchi la ufundi kuwa makini na maamuzi hayo yaliyofanywa na washauri wa Zahera na ajaribu kufuatilia mapungufu yote yaliyojitokeza kwenye mechi na Stand ili kikosi kiwe vizuri.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic