September 25, 2018


Wakati mashabiki wengi wakiwa na hofu juu ya nani ataibuka na ushindi kwenye mchezo wa Simba dhidi ya Yanga Jumapili hii, aliyekuwa Mwenyekiti wa Usajili wa Simba, Zacharia Hans Poppe ameibuka na kusema kuwa ana uhakika asilimia 120 ya wao kuifunga Yanga.

Simba inay­onolewa na Mbelgiji, Patrick Aussems, Juma­pili hii itakuwa na kibarua cha kuwakabili watani wao wa jadi Yanga kwenye pambano la Ligi Kuu Bara katika Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Mara ya mwisho kukutana kwa timu hizi zilizojikusanyia mamil­ioni ya mashabiki wa soka hapa nchini, Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na kiraka Erasto Nyoni.

Hans Poppe ambaye yupo nje ya nchi, amesema: “Asilimia 120 Simba atashinda mechi yake mbele ya Yanga hiyo siku wakiku­tana. Nasema hivyo kwa sababu Simba wamekusanya wachezaji bora na wazuri kuliko wale ambao wapo kwa upande wa Yanga.

“Kwenye nchi ya vipofu chongo ni mfalme, wao wa­namsifia Makambo (Heritier) pekee wakati ukiangalia Simba hapa kuna Kagere (Meddie) ukigeuka huku Okwi (Emmanuel) kati Bocco (John) na Kichuya (Shiza), wakati wao wanamtaja mchezaji mmoja pekee sisi tunataja kikosi kizima.”

3 COMMENTS:

  1. Hatuna tabia ya kucfia cc yanga waambie wamkabe makambo wakione cha moto tunawachezaji waxio julikan hats kuwakaba inakuwa xhida we jifiche tu ya bongo xoka waachie makocha

    ReplyDelete
  2. Huyu si anatafutwa sasa serikali si iwafate nyie mloandika mseme yupo wapi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic