September 3, 2018


Mholanzi anayelipwa Sh.22.7Milioni kwa mwezi na Azam, Hans Pluijm ameweka wazi kuwa ubingwa wa msimu huu si kipaumbele cha waajiri wake. Lakini ni kama anawazuga Simba na Yanga.

Azam ambayo ina uwanja wa kisasa unaokubalika na Fifa, imeanza vizuri ligi ya msimu huu kwa kushinda michezo yote miwili waliyocheza dhidi ya Mtibwa FC na Ndanda FC kwenye uwanja wao wa Azam Complex.

“Sijui kama Azam wamenileta kuja kutwaa taji msimu huu, ila kama mwalimu wa timu unahitaji kuonyesha uwezo na mawazo yako kwa wachezaji ili waonyeshe ubora wao binafsi na ubora wa timu,” alisema kocha huyo aliyeing’arisha Singida United msimu uliopita.

“Nafikiri wanahitaji zaidi kuona wachezaji wakicheza kwa kujituma kwa bidii na kuonyesha kuwa wanahitaji kushinda hilo ndiyo jambo bora na kama kutwaa ubingwa kutakuja kuonekana mwishoni mwa msimu,” alisema Pluijim ambaye alipata mafanikio na Yanga.

3 COMMENTS:

  1. Hana jipya kwa Simba kwa maanaa alipokuwa Singida kwa Simba kachezea mara zote.

    ReplyDelete
  2. Atapigwa 4G kama alivyopigwa akiwa kwa walima alizet.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic