September 3, 2018


Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali, amesisitiza kwa kuutaka uongozi wa Yanga kuhakikisha unafanya uchaguzi mpya haraka ili kumpata Mwenyekiti wa klabu hiyo.

Kauli ya Akilimali imekuja tena kutokana na uongozi wa Simba jana kutangaza kuwa itafanya uchaguzi wake Novemba 3 2018 ili kupata viongozi wapya ambao watachukua nafasi za waliomaliza muda wao.

Mzee huyo ameongea kwa jazba akishangaa kuwa mpaka sasa Yanga haijafanya uchaguzi wakati ndiyo ilikuwa klabu ya kwanza kupaswa kufanya hivyo.

Katibu huyo ameeleza kushangazwa na namna Yanga wanachokitaka huku akisema ni jambo la kushangaza kwa maana hata klabu ya Coastal Union tangu iamuliwe na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kufanua uchaguzi ilikamilisha haraka.

Aidha, Akilimali amesema mpaka sasa aliyekuwa Mwenyekiti wao, Yusuf Manji, hajasema kama amerejea na kwa mujibu wake haoni haja ya kumbembeleza mtu ambaye hana nia ya kurejea.

Yanga na Simba zote zilipewa siku 75 za kuanza mchakato wa uchaguzi na TFF na Simba wametangaza jana tarehe rasmi ya uchaguzi huo ambapo fomu zitaanza kutolewa leo kunako makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo Msimbazi, Dar es Salaam.

5 COMMENTS:

  1. Huyu mzee anaonyesha rangi yake halisi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni Kijani na Njano. Ana akili ya kutosha. Anatambua jambo lililojificha haraka. Ni hazina kubwa kwa klabu yetu ya Yanga.

      Delete
  2. Mbona magazeti yanatangaza kuwa yanga imeshapokea millioni mia tatu kutoka Manji na kutokana na hela hiyo Zahera keshapata kiburi na kutangaza ubingwa kwa ushindi ataoupata kwa kila timua itayekaa mbele ya

    ReplyDelete
  3. Sioni sababu ya kufanya uchaguzi Mzee wetu AkiliMali anatutosha kuwa mwenyekiti wetu

    ReplyDelete
  4. Mzee Akilimali anaweza kuwa sahihi kwa vile viongozi wetu wa Yanga hawaweki mambo mengi wazi hata yale ambayo ni hakika, website ya timu ina habari za siku nyingi, inapelekea watu kuandika habari wanazozijua. Hili suala la uchaguzi liwekwe wazi, mkutano mkuu wa timu uliamua Mwenyekiti hakujiudhuru je amerudi kazini baada ya kuwa nje ya ofisi kwa muda mrefu, je katiba inasemaje kuhusu hili? Tuendelee kuishi kwa matumaini mpaka lini?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic