September 29, 2018


Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera raia wa DR Congo, amedai kuuona mapema mchezo wao dhidi ya Simba namna utakavyokuwa na kwamba hana hofu ya wachezaji wake juu ya kuibuka na pointi tatu kama watatekeleza maagizo aliyowapatia. 

Kwa mara ya kwanza msimu huu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, Zahera atakutana na Simba tangu aanze kukinoa kikosi cha Yanga.

Zahera alisema kuwa hana hofu na mchezo huo na wala hawahofii wachezaji wake kuibuka na ushindi kutokana na kwamba alishawaandaa muda mrefu kisaikolojia juu ya mechi hiyo ambayo anaiona kama inapigiwa kelele nyingi kama vile inatofauti na michezo iliyopita.

“Mimi ninachojua mechi ya Jumapili ipo sawa na mechi zingine zote tulizocheza na kuibuka na pointi tatu, kwa maana hiyo basi sioni kama kuna jipya siku hiyo zaidi ya kutambua tu kuwa mchezo huo ni muhimu kuweka heshima kwa wapinzani wetu na ndiyo maana nilishawaandaa wachezaji mapema.

“Mazoezi tunayofanya yanatosha kabisa kujua nini tutapata katika mchezo huo hasa kama wachezaji wangu watafuata maelekezo yote niliyowapatia, lakini mbali na hivyo, nina imani na uwezo wa mchezaji mmoja mmoja na uelewaBwao, hivyo sina shaka hata kidogo japo natambua ugumu wa mchezo wenyewe ukilinganisha na pointi walizonazo wapinzani wetu,” alisema Zahera.

Awaambia Yanga wasiogope hata kidogo! Zahera ameongeza kuwa, anataka kushuhudia mashabiki wengi wakijitokeza uwanjani kwa ajili ya kuwashangilia vijana wake ili kutimiza lengo la ushindi. “Kwanza kabisa watu wafahamu kuwa, mimi maandalizi ninayoendelea kuyafanya ya timu yangu siyo kwa ajili ya Simba pekee, timu yangu ninaiandaa kwa ajili ya kupambana na kila timu.

“Ninawaomba mashabiki wa Yanga wajitokeze kwa wingi katika mchezo huo tena wasiwe na hofu, kwani hakuna kinachoshindikana kwetu,” alisema Zahera. Adai ameisoma Simba muda mrefu “Muda mrefu sana tumekuwa tukiwafahamu Simba kwa sababu tumewaangalia kwenye michezo mingi namna ambavyo wanacheza.

Siyo michezo ya ligi pekee ambayo tumewaangalia bali tangu wanacheza na Asante Kotoko tuliwaangalia pamoja na wachezaji wote na kuwaonyesha baadhi ya vitu juu ya wao. “Lengo ni kwamba tujue namna ambavyo wanacheza kimbinu na falsafa zao, hakuna kitu ambacho tumekosa kukiangalia kwa Simba,” alisema.

2 COMMENTS:

  1. Ni rahic kuongea kwa maneno kuliko vitendo kikubwa utambue kua ni vigumu kumukamata Simba kwa mikono Unless Utapata tabu xana

    ReplyDelete
  2. ungekuwa mchezo wa kawaeda msingeenda kupiga kambi morogoro wenzenu wamebaki hapahapa subiri dkk 90 ziishe ndio utawajua simba vizuri

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic