September 23, 2018




Beki Mganda wa Singida United, Shafiq Batambuze, amegoma kurejea nchini Tanzania kwa kile kinachodaiwa kuwa ni suala la kutolipwa mshahara na kumaliziwa fedha za usajili, mpaka sasa akiwa yupo kwao Uganda.

Tayari kuna taarifa kwamba Batambuze ameanza mazungumzo na mabingwa wa Kenya, Gor Mahia ili ajiunge nao.

Mganda huyo alisajiliwa msimu uliopita na kikosi hicho na kuwa ni mmoja wa mabeki ambao waliibeba Singida na kumaliza katika nafasi ya tano kwenye msimu wao wa kwanza wa ligi hiyo.


Habari za ndani zinadai kuwa mchezaji huyo tangu msimu huu uanze hajacheza hata mchezo mmoja na kwa sasa yupo kwao Uganda wakati timu yake inaendelea na ligi kuu.


“Kweli Batambuze kwenye timu hayupo kwa muda sasa na inadaiwa kuwa anaudai uongozi fedha zake za usajili pamoja na mishahara na sasa yupo kwao Uganda na hajacheza mchezo wowote wa ligi kuu mpaka,” kilisema chanzo.


Kwa upande wa Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sanga alipoulizwa alisema: “Hakuna tatizo lolote kati yetu na Batambuze ni makubaliano yetu tu na mchezaji yupo kwao na anaendelea na mazoezi kama kawaida.”

SOURCE: CHAMPIONI

1 COMMENTS:

  1. TFF ni jambo la heshima kwa chi yetu kuona aibu ya namna hii hazitokei na kuaibisha taifa letu lakini pia kusimamia haki za wachezaji. Kama ni kweli mchezaji anadai haki yake, simamieni alipwe.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic