September 5, 2018


Ikiwa leo ni siku ya tatu tangu kufunguliwa kwa dirisha la kuchukua fomu za kugombea nafasi mbambali za uongozi katika klabu ya Simba, unaambiwa mpaka kufikia jana hakuna aliyewasili kuchukua fomu.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa klabu hiyo, Boniface Lyamwike, amesema kuwa mpaka kufika jana hakukuwa na mgombea yoyote aliyewasili kunako makao makuu ya klabu kuchukua fomu.

Kinachoonekana kama kuna mtegeano baina ya wanachama wa klabu hiyo ambapo mpaka sasa wadau na wapenzi wa Simba wanasubiria kwa hamu kujua majina yaliyowasili kuchukua fomu za kugombea.

Lyamwike alitangaza kuwa Simba itafanya uchaguzi wake Novemba 3 2018 ili kupata nafasi za Wajumbe wa Bodi ambao utachukua muda wa wiki moja pekee.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic