KAGERA KUIKOSA MILIONI MOJA YA MCHEZAJI BORA AGOSTI
Na George Mganga
Straika mwenye balaa la aina yake katika klabu ya Simba, Meddie Kagere, yuko kwenye hatihati ya kuikosa zawadi ya kitita cha shilingi za kitanzania, milioni moja kutokana na kukosekana kwa mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu Bara.
Zawadi hiyo ambayo ilikuwa inatolewa na Vodacom kama wadhamini wakuu waliopita sasa itakuwa ngumu kwa Kagere kuipata kwa wakati baada ya Shirikisho la Soka Tanzania kukosa mdhamini wa ligi hadi sasa.
Kagere alitangazwa jana kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu kwa mwezi Agosti ambapo anapaswa kukabidhiwa zawadi ya milioni moja za kitanzania pamoja na king'amuzi cha AZAM TV.
Straika huyo sasa atajibebea king'amuzi pekee badala ya vyote kwa mpigo mpaka pale TFF itakapompata mdhamini mkuu wa mashindano hayo.
Hivi karibuni TFF kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Wilfred Kidao, alisema wanaendelea kuzungumza na makampuni mbalimbali kwa ajili ya kumpata mdhamini huku akiahidi kuwa atapatikana wakati ligi ikiwa inaendelea.
MK 14 mtunzieni mali zake.. atakusanya sana
ReplyDelete