KIGOGO SPUTANZA AINGIA KALI SAKATA LA SINGIDA NA MANYIKA, AIGUSIA TFF
Kufuatia sakata la kipa aliyebakiza mkataba wa mwaka mmoja na Singida United, Manyika Peter kujiweka kando, Mwenyekiti wa Chama cha Kutetea Haki za Wachezaji nchini (SPUTANZA), Mussa Kisoki, ameitaka TFF kuwa karibu na wachezaji.
Kisoki ameeleza kuwa TFF ndiye mama wa soka la Tanzania japo imeshindwa kupata njia stahiki za kuwasaidia wachezaji wa klabu za Tanzania.
Kisoki amesema hayo kutokana na wachezaji wengi wamekuwa wakishindwa kulipwa stahiki na vilabu vyao hapa nchini, jambo ambalo limekuwa likipelekea malalamiko kuwa mengi.
Mwenyekiti huyo amelitaa shirikisho kuhakikisha inajaribu kuwa karibu na wachezaji ili kuepuka kutolipwa stahiki zao ikiwemo fedha za mishahara haswa kwa baadhi ya vilabu ambavyo havifanyi hivyo.
Manyika ameamua kujiweka kando na Singida United kwa kushindwa kulipwa fedha zake za usajili tofauti na makubaliano ya mkataba wao namna yalivyokuwa.








0 COMMENTS:
Post a Comment