MMOJA ATEMWA STARS SABABU YA MAJERAHA
Na George Mganga
Beki wa kati wa klabu ya Yanga na Taifa Stars, Kelvin Yondani. ameondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa kufuatia kupatwa na majeraha ya mguu.
Yondani sasa ataukosa mchezo ambao Stars ambayo itacheza dhidi ya Uganda Septemba 8 wiki hii kwenye Uwanja wa Nambole huko Kampala.
Mchezaji huyo ameumia mguu na kwa mujibu wa daktari wa timu ameshauri ni vema akasalia nchini kwa ajili ya matibabu zaidi.
Wakati huo kikosi cha Stars kinaondoka leo nchini kuelekea huko Kampala tayari kukipiga na Uganda kwenye kipute cha kufuzu kuelekea AFCON 2019.
Uganda inakutana na Stars ikiwa na wachezaji kadhaa ambao wanacheza soka hapa nchini wakiwemo Emmanuel Okwi (Simba) na Nicolous Wadada (Azam FC).








0 COMMENTS:
Post a Comment