September 21, 2018


Baada ya kuambulia kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Mbao FC jana kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, uongozi wa Simba umetaka mechi yao dhidi Biashara isogezwe mbele.

Kwa mujibu wa Kaimu Rais wa klabu hiyo, Salim Abdallah, amesema wametuma maombi kwenda Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutaka mchezo wao na Biashara usichezwe Septemba 27 2018.

Abdallah amesema wametuma maombi ya kuomba mechi hiyo isogezwe mbele ili kuwapa nafasi ya kujiandaa na mechi ya watani zao wao wa jadi Yanga itakayopigwa Septemba 30.

Kiongozi huyo ameeleza kama ratiba hiyo itaendelea kusalia hivyo itazidi kuwanyima nafasi ya kujiandaa vema kutokana na ratiba kuwabana hivyo wamependekeza vema wakapata muda mzuri.

Simba na Yanga zitakutana Uwanja wa Taifa Septemba 30 2018 ikiwa ni kibarua cha kwanza kwa msimu huu kwa timu hizo mbili kukutana.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic