September 16, 2018


Baada ya kushindwa kuipandisha kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, Kocha wa Dodoma FC, Jamhuru Kihwelo 'Julio', amesema ataachana rasmi na kazi hiyo endapo atashindwa kuipandisha tena msimu ujao.

Kocha aliyewahi kusema anapenda zaidi sifa kuliko pesa, ameibuka na kufunguka hayo baada ya kukosa nafasi hiyo msimu wa mwisho wa Ligi Daraja la Kwanza.

Julio ameeleza kuwa haoni tena nafasi ya yeye kuendelea kuwa Kocha kama atashindwa kuipelekea Dodoma FC kwenye ligi msimu ujao.

Kocha huyo ambaye amewahi kuwa Msaidizi katika klabu ya Simba na mara mwisho akiwa na King Kibaed Mputa, ameamua kuweka hadharani malengo yake akiwa na Dodoma FC na endapo timu isipopanda daraja ataacha rasmi kazi hiyo.

4 COMMENTS:

  1. Acheni kuiba picha za Simba kuwasilisha mada isuowahusu ni uandishi gani huu?

    ReplyDelete
  2. saleh naona umechoka mbona uwandishi wako haueleweki

    ReplyDelete
  3. Jinga tu hili liandishi. Halina hata chembe ya maadili ya uandishi wa habari.


    ReplyDelete
  4. Jiheshimu mkuu! Tunapenda hii blog ila Kwa hizi habari za kindezi tutaanza kuhama! Title : KOCHA SIMBA KUJIENGUA halafu ndani habari inamuhusu kihwelu huo huo si upimbi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic