Taarifa kutoka Simba imesema tayari wanachama wote waliokuwa wamechukua fomu wamesharudisha ili kupisha hatua nyingine inayofuata.
Uongozi huo umeeleza kuwa zoezi linalofuata hivi sasa ni mchakato wa usaili wa fomu hizo ambao utafanyika kesho Jumatatu.
Zoezi hilo litafanyika kabla ya kuelekea kampeni ambapo kila mwanachama ataruhusiwa kunadi sera zake kwa ajili ya kuwavutia watakaowapigia kura.
Ikumbukwe Simba itafanya uchaguzi wake mkuu Novemba 3 2018 ili kuwapata viongozi wengine watakaoongoza klabu hiyo kwa miaka minne ijayo.








0 COMMENTS:
Post a Comment