KOCHA SIMBA AZISHUHUDIA COASTAL UNION NA LYON JUKWAANI LEO
Na George Mganga
Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma, leo alikuwa Uwanja wa Uhuru kuzishuhudia timu za African Lyon na Coastal United zikicheza mchezo wa ligi.
Djuma yupo jijini Dar es Salaam kuendelea na majukumu ya kuwanoa wachezaji wa kikosi cha Simba kilichosalia kwa ajili ya mechi zijazo za ligi.
Ikumbukwe hivi karibuni ilielezwa kuwa Djuma angeweza kondoka klabuni hapo lakini uongozi wa Simba uliibuka juu na kusema hawana mpango wa kuachana naye.
Wakati Djuma akiwa Uwanja wa Uhuru leo, kikosi cha Simba kipo mjini Mtwara kwa ajili ya kibarua dhidi ya Ndanda FC kesho Jumamosi.
Simba itakuwa ugenini kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona kucheza dhidi ya walima korosho hao ambao wametamba kutengua rekodi ya kutowafunga Simba tangu wapande daraja kushiriki Ligi Kuu 2014.
Sasa nimewaelewa Simba kwanini wamemuacha kocha msaidizi Daresalam.Simba wapo kimkakati zaidi tofauti na tunavyofikiria na kweli wamedhamiria kuutetea ubingwa wao.
ReplyDeleteTimu inataka wachezaji wote hata waliobakia Där wawe fit chini ya kocha Djuma wengine wamekalia majungu. Simba ndio waajiri na ndio wanahaki ya kumpangia kazi.Djuma ana mshahara mkubwa kuliko makocha wakuu wa timu zote za ligi kuu Tanzania ilipokuwa kocha wa Azam pekee. Ndio thamani aliyonayo Simba.
ReplyDeletesasa mbona alikua uwanjani anaangalia mpira au hayo mazoezi walikua wanafanya usiku
ReplyDeletesasa mbona alikua uwanjani anaangalia mpira au hayo mazoezi walikua wanafanya usiku
ReplyDelete