NILIONDOKA KAMA MKIMBIZI, NILIAZIMA ADA YA MWANAFUNZI – VIDEO
Mwanamasumbwi Hassani Mwakinyo aliyeweka historia baada ya kumtwanga Muingereza, Sam Eggington, leo ametembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwaahidi Watanzania kuwa hawatawaangusha katika mashindano mengine ambayo yapo mbele yake.
Akizungumza na wanahabari nje ya ukumbi wa Bunge hilo jijini Dodoma, Mwakinyo amesema jambo ambalo hatolisahahu katika ushindi huo wa juzi ni pale alipiokuwa akitafuta visa kwa ajili ya kusafiri kwenda Uingereza kwenye mpambano huo.
“Nimeondoka Tanzania kama mfungwa, kama mkimbizi, hata pesa ya kulipia visa ilikuwa shida kuipata, nakumbuka hata nauli tu ilibidi nikope pesa ya ada ya mwanafunzi.
“Nimepigana Uingereza bila sapoti yoyote, lakini namshukuru Mungu nimeshinda, wapo wengi wanasema ni mameneja wangu, niseme tu kwamba ni waongo, hakuna mtu anayenimeneji, wala aliyetoa pesa yake mfukoni kunigharamaia,” amesema Mwakinyo.
Hongera sana sana khasan. Ulishinda uiengereza na unaendelea kushinda hapa nyumbani kwa kuwa muwazi ingawa kuna watakaochukia lakini msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Kuna uozo mkubwa kabisa katika vyama vyetu vya michezo. Matatizo yaliokuwepo kwenye ngumi ndio yaliyokuwepo kwenye riadha na kadhalika. Serikali licha ya jitihada kadhaa wa kadhaa katika sekta mbali mbali lakini bado hawaichukilii michezo kama sekta mama na muhimu kwa maendeleo ya nchi. Nasema sekta mama kwa sababu ni sekta inayoajiri vijana wengi ambao ndio idadi kubwa ya watanzania.
ReplyDeleteWadau tulishapiga kelele sana mpaka tukamuachia Mungu kuwahimiza wahusika kuipa umuhimu sekta ya michezo sawa na sekta ya utalii katika jitihada za kuitangaza nchi. Tumejionea wenyewe dakika 15 za khasan Mwakinyo jinsi zilivyoitangaza Tanzania. Maisha ni kupanaga na kupanga ni kuchagua.kwa nchi kama Tanzania inaweza kuhangaika kutumia rasilimali kubwa kuutangaza utalii wake na tukafeli kwani nchi tajiri duniani licha yakuwa hazina vivutio bora vya asili vya kitalii lakini kwakutumia nguvu zao za pesa wana uwezo wa kuvitangaza vibaya vya kwao na vikaonekana bora na hatuwezi kushindana nao na ndipo linapokuja wazo la kutumia vipaji vya wanamichezo kuitangaza nchi ambapo ni sawa na kuua ndege wawili kwa kutumia jiwe moja. Kudhalisha ajira kwa vijana na wakati huohuo wakiitangaza nchi kimataifa. Kwa wenzetu waliosiriasi wizara ya michezo ni ni wizara kamili inayojitegemea. Kwa sababu vyama vyetu vya muchezo vimeoza utaona hata khassan hakufikiria kwenda kuomba msaada wakati anaelekea Uingereza. Kwa kiasi fulani ni aibu kwa jinsi mambo yanavyokwenda lakini tutafanyaje ila tunategemea suala la khassan litawaamsha wahusika. Khassan ni dhahabu inayosafiri bila mwangalizi na bila kuwa na mwenywe uzembe huu utakoma lini?
wizara yetu ilikuwa wapi vipaji hivi
ReplyDelete