September 18, 2018


Baada ya juzi Jumamosi Simba kubanwa na Ndanda, kocha mkuu wa kikosi hicho, Patrick Aussems, raia wa Ubelgiji, ameibuka na kusema kuwa, kama viwanja vingine vya mikoani vitakuwa na ubora wa chini kama ilivyo kwa Nangwanda Sijaona, basi kuna hatari kwao ya kupata ushindi.

Kauli ya Aussems imekuja muda mfupi baada ya kuk­ishuhudia kikosi chake kik­ishindwa kufungana na Ndanda katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.

Kabla ya mchezo huo wa juzi, Simba ilicheza uwanjani hapo dhidi ya Ndanda mara nne na kushinda mechi zote, lakini juzi Jumamosi kwa mara ya kwan­za imeshindwa kupata ushindi, huku Aussems akiulalamikia uwanja kuto­kuwa na ubora.

Kwa mujibu wa Cham­pioni Jumatatu, Aussems alisema: “Kama kutakuwa na viwanja vingi vya aina hii, basi itakuwa tatizo kubwa kwetu kupata ushindi tuk­ienda kucheza huko. Uwanja huu hauna ubora kabisa.

“Nawapongeza Ndanda kwa kupata sare hii kwani tangu mwanzo wa mchezo wao wali­ingia wakiwa na nia ya kujilinda zaidi kuliko kushambulia na wakafanikiwa kwa hilo. Hivi sasa tunajipanga kuangalia tunapata matokeo mazuri katika mechi zijazo.”

Simba baada kucheza na Ndanda juzi, Alhamisi ijayo itakuwa Mwanza kupambana na Mbao FC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, kisha itaenda Shinyanga kucheza na Mwadui kwenye Uwanja wa Kambarage.

3 COMMENTS:

  1. Huyu kocha nae asitie kichefuchefu hapa, Simba huwa haangali pa kuwindia pawe kichakani au kwenye nyasi lazima ataua tu. Kocha akae na wachezaji wake wajitathmini maana inaonekana hawaeleweki wala hawajielewi kutokana na jinsi wanavyocheza. Nani aliwaambia kuwa wachezaji wajilegeze kama wadada halafu wakachukue ushindi mbele ya wanaume yaani ujinga mtupu wachezaji wenye matunzo mazuri kwenye klabu yao wanashindwa kuonesha thamani yao badala yake wanakwenda kuwaruhusu wachagani wapate sifa za bure kabisa kwa kuwatumia wao .Wanachama na wapenzi wa Simba sihaba wanaiunga timu yao mkono kila inapokwenda lakini wachezaji wanawaungusha kiasi cha kutia aibu. Wachezji wanatakiwa kuwa serious na kuonesha tofauti kati ya bingwa na wanaojarbu kuwa bingwa la sivyo kauli ya Magufuli itabakia na ukweli wake kuwa Simba bado kwani kama inashindwa kushinda vitimu vya mchangani basi waache kabisa kuifikiria TP MAZEMBE na vigogo wengine wababe wa Africa.

    ReplyDelete
  2. Hugo cocha Nate ameshafel. Ati viwanja vibovu in vigumu kupata ushindi? Kwanini asiulize msimu uliopita ilikuwaje simba wakashinda kwenye viwanja hivyo ambavyo yeye Leo ndiyo anaviona vibovu na wachezaji ni wale wqle

    ReplyDelete
  3. Wazungu wajanja sana aisee. AMEKUJA KWA TIKETI YA UKOCHA KUTALII nchini kwetu halafu tunamlipa mahela kibao, hatupo serious. Sio kocha huyo TIMUAAAA

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic