September 7, 2018


Na George Mganga

Kuelekea mechi ya dhidi ya Uganda, Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Hemed Morocco, amewaahidi watanzania kutegemea maajabu Septemba 8 2018.

Morocco amesema kwa namna maandalizi ya mchezo huo namna yalivyoeanda tangu kikosi kikiwa Dar es Salaam kuna uwezekano mkubwa wa kupata matokeo wakiwa ugenini.

Kocha huyo ana imani Stars inaweza kuibuka na ushujaa mbele ya Waganda kwa kuchagizwa na wachezaji wengi wanaocheza soka la kulipwa nje ya Tanzania.

Stars itakipiga na Uganda Septemba 8 kwenye Uwanja wa Nambole jijini kampala, ukiwa ni mchezo wa kufuzu kuelekea AFCON 2019.

Tayari kikosi cha Stars kimeshawasili tangu jana jijini Kampala na sasa kinachosubiriwa ni mchezo huo Jumamosi hii.

1 COMMENTS:

  1. TUNANAKUAMINI KOCHA WETU MANENO YAKO YATIMIE KWA TIMU HII TUTEGEMEE MAAJABU SEPTEMBA 8 2018. ASANTE KOCHA MOROCCO.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic