September 1, 2018


Na George Mganga

Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, amempongeza Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike kutokana na maamuzi yake ya kuwasamehe wachezaji wa Simba.

Amunike amewasamehe wachezaji hao 6 baada ya kuchelewa kuripoti kambini kwa ajili ya kuanza mazoezi na Taifa Stars kuelekea mechi ya kufuzu AFCON dhidi ya Uganda huko Kampala.

Baada ya kuwasamehe, Rage ameibuka na kumpongeza Amunike kwa kusema amefanya kitendo cha kiungwana akieleza kuwa ni jambo jema.

Rage alishauri ni vema Kocha akakutana na wachezaji au TFF ili kuzungumzia suala hilo kabla ya kutoa adhabu kwa wachezaji hao ambao wamekuwa wakiitwa mara nyingi Stars.

Hata hivyo licha ya kusamehewa, wachezaji hao wataukosa mchezo huo utakaopigwa Septemba 9 huko Kampala kutokana na nafasi zao kuchukuliwa na wachezaji wengine.

6 COMMENTS:

  1. YALIKUWA MAAMUZI MABAYA BAD START

    ReplyDelete
  2. Walihukumiwa wa kosa lipi na kanuni gani?Kuripoti timu ja taifa kwa mujibu wa kanuni za FIFA ni saa 72 au siku 3 kabla ya mechi. Kina Samatta,Banda nä Msuva walitakiwa kuripoti leo wamesharipoti?Watatimuliwa?Wacheni uswahili fuateni kanuni sio ushabiki wa vijiwe vya kahawa.

    ReplyDelete
  3. Yaani, uitwe Leo, ww useme SAA 72?

    ReplyDelete
  4. Yaani, uitwe Leo, ww useme SAA 72?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic