September 3, 2018


Huenda ikawa habari njema kwa Yanga na mbaya kwa mashabiki wa Simba. Ni baada ya mshambuliaji wa Wanajangwani, Heritier Makambo kutarajiwa kuanza mazoezi na timu hiyo, akitokea kwenye majeraha.

Mshambuliaji huyo alipata maumivu ya misuli kwenye mchezo uliopita wa Kombe la Shirikisho Afrika wakati timu hiyo ilipocheza na Rayon Sports ambao ulimalizika kwa Yanga kufungwa bao 1-0, hivi karibuni. Katika mchezo huo, Makambo alishindwa kumalizia mechi hiyo na kutolewa dakika ya 69 baada ya kugongwa na goti kwenye sehemu ya msuli wa paja.

Kwa mujibu wa gazeti la Championi, Zahera alisema mshambuliaji wake huyo tegemeo tayari amemaliza siku nne za mapumziko alizopewa na daktari wa timu hiyo, Edward Bavu. Zahera alisema, kwa kuanza atafanya mazoezi mepesi binafsi kwa muda wa siku mbili kabla ya kuanza magumu na wenzake siku ya tatu baada ya kuwafiti kwa asilimia 100.

Aliongeza kuwa, kurejea kwa mshambuliaji huyo kumempa matumaini ya kuendelea kupata ushindi katika michezo ijayo kutokana na umuhimu alionao mchezaji huyo kwenye safu yake ya ushambuliaji.

“Nilisikitika kuumia kwa Makambo kwenye mechi dhidi ya Rayon, beki wa Rayon alimgonga kwa makusudi kwa lengo la kumuumiza na ninaamini alifanya hivyo baada ya kumgundua ni mchezaji hatari.

“Sikutaka kumtoa katika mechi hiyo na nili_ kia maamuzi ya kumtoa kwa hofu ya kumuongezea maumivu zaidi, hivyo nikaona nimtoe kwani mchezo huo haukuwa na kitu cha kupoteza zaidi ya kukamilisha ratiba. Hivyo, Makambo amemaliza muda wa kupumzika alliopewa na daktari aliokuwa akiutumia kwa ajilli ya matibabu pekee,” alisema Zahera.

Makambo anatarajiwa kuwa mwiba mkali kwa Simba wakati watani hao wa jadi watakapokutana Septemba 30 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Wakati huohuo, Juma Abdul na Juma Mahadhi wamerejea na wataanza mazoezi leo Jumatatu kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi. Juma alikuwa anasumbuliwa na enka alipoumia katika mechi dhidi ya Mtibwa, wakati Mahadhi alikuwa akisumbuliwa na goti baada ya kuumia katika mechi dhidi ya USM Alger.

6 COMMENTS:

  1. Hahaaaaaa inamaana makambo ni kwa simba tu akili mbovu hiyo

    ReplyDelete
  2. Mambo mengine ni upuuzi . Waandishi wa bongo wakati mwengine kama wanaugua ugonjwa wa akili. Mwandishi anaposukumwa na upenzi au kibiashara zaidi kuliko uhalisia wa mambo kwa kile anachokiandika siku zote huwa kama ujinga fulani hivi.Habari mbaya kwa Simba kwa Makambo? Kwa mpangilio na maandalizi na utamamu wa timu Yanga na makambo wao unaipa nafasi mbele ya Azam? Ukiangalia pale Simba kuna makambo wangapi? SIMBA hata hawamfikirii Makambo.Kama Kagere alivyouliza kwani Makambo ndio nani? Kwanini asije Boko wa kuhofiwa zaidi kwani amethibitisha mara kadhaa kwenye ligi ya bongo kuwa anauwezo wa kuifunga timu yeyote ile. Ikiwa habari mbaya kwa Simba kwa Makambo mmoja kutakuwa habari gani Nzuri kwa upande wa Yanga kutoka kwa akina Kagere, Dilunga na wakali wengine?

    ReplyDelete
  3. Makambo yupo Level ya wakinasalamba kaheza bado hajawafikia kiwango wakina bocco kagere okwi bado sanaaaa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wew usimfananishe Salamba na mambo ya ajabu... Makambo hana hata sifa za kuichezea SIMBA... Anavyokimbia tu utazania ni kilema.

      Delete
  4. Mnaandika eti beki wa Rayon alimuumiza makusudi baada ya kugundua ni mshambuliaji hatari. Tulioangalia mechi ile hatukuona hatari yoyote ya Makambo. Hakuwa tishio Kwa Rayon hata kidogo mpaka alipotolewa. Ushabiki huu wa mwa magazeti ni tatizo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic