September 3, 2018


Kiungo wa timu ya Taifa Stars, Himid Mao, anatarajiwa nchini kesho mchana Septemba 4 nchini tayari kuungana na kambi ya Stars.

Mao atawasili jijini Dar es Salaam na shirikila la ndege la Ethiopia ili kuungana na wenzake ambao wanaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Boko Veterani jijini humo.

Awali iliarifikwa kuwa Mao angeweza kuwasili leo lakini kutokana na mambo kuingiliana imebidi atue nchini kesho.

Wakati Mao akitarajiwa kuwasili, kikosi cha Stars bado kinaendelea na kambi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kufuzu kuelekea AFCON 2019 dhidi ya Uganda.

Stars wanakipiga na Uganda Septemba 8 huko Kampala kuanza safari ya kuwania tiketi ya kucheza mashindano hayo mwakani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic