September 20, 2018


Mshambuliaji tegemeo wa Yanga Mkongomani, Heritier Makambo amewaambia mabeki wa timu pinzani waendelee kumchezea kwa kumpania, lakini atafunga tu mabao.

Kauli hiyo ameiibua jana mara baada ya kutupia bao moja na pekee dhidi ya Coastal Union ya Tanga katika mchezo ambao waliibuka na ushindi wa bao hilo pekee.

“Siku zote hakuna beki anayekubali kupitwa kirahisi na mshambuliaji na kwenda kufunga bao, ni lazima beki apambane kukuzuia wewe mshambuliaji ili usifunge.

“Hivyo, kwangu sioni cha ajabu kuona mabeki hao wakija uwanjani kwa ajili ya kunifuata kunizuia zaidi ninajipanga kuhakikisha ninakabiliana nao kuifungia timu yangu mabao,” alisema Makambo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic