May 1, 2018



Baadhi ya wanachama wa tawi la klabu ya Yanga kwa Motogole, wameeleza kusikitishwa na Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa kutokana na kupoteza mchezo wa juzi dhidi ya Simba wakisema yeye ndiye chanzo.

Mmoja wa viongozi wakubwa ndani ya tawi hilo, amesema kuwa Nsajigwa amewasaliti akidai alitumika mpaka kusababisha Yanga ipoteze kwa bao 1-0 dhidi ya watani zao wa jadi, Simba.

Yanga ilifungwa mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa bao 1-0 na kujiwekea mazingira magumu ya kuendelea kuutetea ubingwa wa ligi.

Akizungumza kupitia Radio One jana jioni, Kiongozi huyo aliye na mamlaka makubwa ndani ya tawi hilo alieleza kuwa Nsajigwa alitumika kutengeneza matokeo huku akimtupia lawama akiuomba uongozi watafute mbadala wake akidai kuwa wakati wake umefikia mwisho.

Baada ya matokeo hayo, Yanga sasa imeweka nguvu zake zote kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya U.S.M Alger utakaopigwa Mei 7 huko Algeria.

10 COMMENTS:

  1. Waliotusaliti ni wachezaji watatu tuliowanyangnya Simba bila ya kuwataja majina yao. Inaonesha kopo kitu chinikwachini

    ReplyDelete
  2. Nilishawahi kumwambia Mkwasa mwanzoni kabisa khs Nsajigwa lkn amekuwa kimya mpk hv sasa.

    ReplyDelete
  3. Acheni maneno. Mnaozungumza hayo hamna machungu ya kweli na Yanga yangu. Tutafute mwarubaini kwa mwaka unaokuja. Ukiangalia uwezo wa Wachezaji wetu na ule wa Wenzetu ni tofauti kubwa sana. Mjue hata uzoevu ni wa maana sana uwanjani. Kwa upande wangu vijana walijitahidi goli moja haliniumizi kichwa ni sehemu tu ya mchezo. Bora tuangalie mbele kwenye mashindano ya kimataifa tuache ujinga wa kulaumiana.

    ReplyDelete
  4. Huwezi kumlinganisha Nsajigwa na Pierre wala Djumaa

    ReplyDelete
  5. Kusema eti wachezaji waliosajiliwa toka walisaliti timu ni porojo zisizo na tija,Yanga walijitahidi sana sana na walicheza kwa moyo wote,angalia hata baada ya kuwa 10 tu uwanjani,bao 1 ni sehemu ya game,tuache porojo,tuongee kama watu wanaojua soccer siyo vilaza.

    ReplyDelete
  6. Kama mna hakika wamekusalitini wafukuzeni wakatafute maisha kwenginrko. Wachezaji hao kwa mapenzi yao juu ya yanga wameikacha simba iliyowalea leo mnawaita wasaliti

    ReplyDelete
  7. Jamani kwa wachezaji 10 uwanjani mnasema mmesalitiwa? Mbona goli halikuongezeka kama usaliti upo, hebu tuwe na hoja za kusaidia timu zetu na wala siyo kulalamika.

    ReplyDelete
  8. Kwa kikosi hiki chenye majeruhi kibao mnashangaa na matokeo haya. Kubalini matokeo ni sehemu ya mchezo au mlitaka mfungwe goli nane ndipo mjue kikosi kina matatizo.Sasa tumieni hizo millioni 600 kuimarisha kikosi chenu ili mtuwakilishe vizuri kwenye michuano ya kimataifa. Kila la kheri

    ReplyDelete
  9. nilidhani mtaanza na 'KAMATI YA UFUNDI'...................

    ReplyDelete
  10. Hata hivyo Nsajigwa hawezi kupambana na Ilambona wala Pierre kwenye 3:5;2

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic