Dakika 90 zimekamilika Uwanja wa Nelson Mandela, Simba inayeyusha pointi tatu mbele ya Prisons ikiwa ni mchezo wake wa kwanza kupoteza ndani ya msimu wa 2020/21.
Inabaki na pointi zake 13 kibindoni na imefungwa jumla ya mabao matatu baada ya kucheza mechi sita ndani ya ligi.
Inashushwa na Yanga ambayo imeshinda leo mbele ya Polisi Tanzania, Uwanja wa Uhuru bao 1-0 na kufikisha pointi 16.
Kipindi cha pili kimeanza, Rukwa
Zimeongezwa dakika 3
Dakika ya 90 Mbangula anaonyeshwa kadi ya njano
Prisons 1-0 Simba
Dakika ya 70 Simba bado ipo nyuma kwa bao moja huko Rukwa.
Dakika ya 61 Ilanfya anatoka anaingia Sheva
Dakika ya 58 Ilanfya anashindwa kufunga bao ndani ya 18 akiwa na mlinda mlango Jeremia Kisubi.
Dakika ya 56 Kimenya anapeleka hatari kwa Manula.
Dakika ya 55. Mashilindi anaonyeshwa njano kwa kmchezea rafu Luis.
Dakika ya 54 Manula anaokoa shuti la pili lilipigwa na Mashilindi.
Dakika ya 48, Samson Mbangula anafunga gooool kwa kichwa
Hakuna mabadiliko kwa timu zote mbili kwa sasaTanzania Prisons 0-0 SimbaUwanja wa Nelson Mandela, Rukwa.
Mapumziko
Tanzania Prisons 0-0 Simba
Uwanja wa Nelson Mandela
Dakika 5 zimeongezwa
Tanzania Prisons imecheza jumla ya faulo 11 na Simba imecheza faulo 7
Dakika 45 zimekamilika
Dakika ya 35 milango bado migumu kwa timu zote mbili.
Dakika ya 31 Erasto Nyoni anaokoa hatari
Dakika ya 22 Tanzania Prisons wanafanya shambulio la hatari lango la Simba, mwamuzi anasema kuwa wameotea.
Dakika ya 18: Simba wanapiga kona ya pili zote hazizai matunda ndani ya uwanja kupitia kwa Bernard Morrison
Dakika 15 zinakamilika na hakuna timu iliyoona lango la mpinzani.
Mpira ni wa nguvu nyingi kwa nyingi, Tanzania Prisons wanawapa tabu Simba Uwanja wa Nelson Mandela. Luis anapewa huduma ya kwanza.
Dakika ya 14, Shomari Kapombe anakwenda nje kwa kuwa ameumia anaingia Kenedy Juma.
Kipindi cha kwanza:-Ilanfya anaotea kwa Simba
Chris Mugalu naye ni miongoni mwa nyota wa Simba ambaye ameripotiwa kupata majeraha
Msimamo wa ligi ukoje?
ReplyDeletePoleni sana Wana Simba. Mpira mliocheza haulingani na usajili mlioufanya.
ReplyDeleteBaelezee hao mikia wenye kujifanya wana kikosi kipana, wapiiiiiii, watupisheeeee
DeleteHata Range Rover brand new na Toyota Land Cruiser V8 new model na ubora wao huwa yanapata pancha
DeleteHata Range Rover brand new na Toyota Land Cruiser V8 new model na ubora wao huwa yanapata pancha
ReplyDeleteLigi inaendelea michezo haijafika hata nusu ya inayotegemewa kuchezwa. Ubingwa bado uko wazi kwa ye yote mbio na ziendelee
ReplyDeleteNiliwambiaga kuwa mashabiki wa simba mpira hauchezwi mdomoni mpira unachezwa uwanjani endeleen kutamba tena mikia fc na mtakoma mwaka huu cc ni mwendo wa moja moja endeleo kufunga saba
ReplyDeleteSimba kachukua ubingwa msimu uliopita kafungwa mechi 4 Wewe unayecheza mpira uwanjani tutakauona muda si mrefu utasikia TFF wanaibeba simba , mara simba wanapulizia dawa vyumbani, mara simba wachwawi tutawaona humu humu na mwaka huu kama hamjakimbilia FIFA sijuiiiiiii
DeleteMan City Man U Liver Pool Nazo Huwa Zinapoteza Tena Kwa Idadi Kubwa Ya Magor Sembuse Simba Ngoja Tusubiri Tuone Huenda Nyie Mkamaliza Lig Bila Kupoteza, Wana Simba Haya Ni Matokeo Ya Mpira Na Haya Zuii Kutetea Ubingwa
ReplyDeleteLiver mwenyewe alipigwa Saba unsshangaa Simba, u to utopolo kicheko kanakwsmbz washakuwa mabingwatyr
ReplyDeleteLiver na mikia wapi na wapi nyie mnajua mpira kuzidi liver na ndo maana mmefungwa 1 wao walifungwa 7 endeleen kucheza mpira mdomon mtakuja kufa na presha mtuletee matatzo tanzania
ReplyDeleteWenye presha ni nyie mnaosusia hadi kushangilia timu ya Taifa, Simba kachukua ubingwa msimu uliopita kafungwa mechi nne, ila nyinyi mnaaoona Ligi imeisha kwa kuwa simba kafungawa jana msije kuilalamikia TFF maana navyo jua mimi chura FC wao wana dhani wana haki ya kushinda kila kitu kwenye mpira wa bongo wakati timu yenyewe ni ya kuunga unga
DeleteSimba bingwa mtetezi bingwa wa nchi, liver bingwa mtetezi bingwa wa nchi. Huyo kiazi utopolo hapo juu hajui mpira anafikiri Simba sawa na utopolo, Hamna kitu hpo aende shule ya kijamii ajifunze
DeleteKufungwa simba ndio mpira ila wasiojua mpira ndio wanao piga kelele.Kama simba angefunga goli moja tu akiwa Dar basi ingeisabika simba kafungwa pia,ila Yanga ushindi wa goli moja sio tatizo. Kagere,Boko,Mugalu,Chama,Kapombe,wawa,Ame,kahata kukosekana ni dhahiri pengo litaonekana hata hivyo Prison walipaki basi na simba hii. Vijana wa simba wamejitahidi ila kocha anatakiwa kumuamini kimeta Duchu kuliko Erasto Nyoni kwani bado hayupo fiti na kwa kiasi kikubwa ndie alieisababushia majanga difence ya simba kwenye mechi ya prison.
ReplyDeleteIko wapi dhana ya kuwa simba ina kikosi kipana? Kikosi kipana Mana yake hata ulifanya rotation ya wachezaji bado wacheze kwenye ubora uleule.
DeleteKutokuwepo kwa chama na wengine ndo tambueni mna kikosi Cha kawaida tu Ila ni kwa vile wamekaa pamoja muda wa kutosha ndo mkatengeneza dhana isiyo na mashiko eti kikosi kipana.
Yuko wapi Morisson mbona Ana ruka ruka tuuuu
Dhana ya kikosi kipana maana yake uwe unashinda kila mechi yani we haufungwi kweli nyie ndio manara anawambiaga tatizo lenu mmeujua mpira kupitia mitandao ya kijamii
DeleteMorrison kafanya mambo yake vzr huoni penati 2 za wazi kasababisha refa kapeta. We kiazi utakufa na kihoro kwa morrison
DeleteTimu za majeshi zingetafutiwa ligi zao,mchezo ulikuwa wa kibabe sana
ReplyDeleteMwaka jana tulivyofungwa na Mwadui waliongea hivi hivi, baaade zikaanza lawama mara TFF WOTE SIMBA, Sasa hivi washasusia mpaka TIMU YA TAIFA wamesahau kwamba ligi ni mbio za marathoni ndio kwanza simba kacheza mechi 6 tu kati ya mechi 34 alafu hao wanaoongea wametuzidi point tatu tu, kwa mtu anayeujua mpira hawezi makelele kwa wale Many**** FC lazima wapige kelele sana
ReplyDeleteteh teh simba bhana wakifungwa wanakua wakali ko mlitaka mfungwe afu tuwasifie acheni hasira jamaniiiiiiiii, matuc ya nin huu ndo mpira
ReplyDeletemnaleta stori za mwaka jana saiv magoli ya offside yameyeyuka naona mikoani mnataabikaa, eti mpira umeongezwa dk 3 refa anachezesha mpga dk 95 na sekunde 43, tulieni dawa iwaingie
ReplyDeleteUtopolo wanalazimisha furaha lakini moyoni wana majonzi kwa kuwa wanajua furaha yao huwa inadumu kwa wiki moja mpaka mbili, kwa hiyo hatuna haja ya kujibishana na nyinyi tunataka kila mechi ya ligi muwe mnakuja ku comment kwenye huu ukurasa
ReplyDelete