MANARA AFAFANUA SIMBA ILIVYOIZIDI YANGA MAKOMBE 9, APINGANA NA NENO BINGWA WA KIHISTORIA
Ni kweli Yanga ni mabingwa mara 27 Tanzania huku Simba ikuchukua mara 19.
Ila kwa makombe yote Tanzania na yale vilabu vyetu vimewahi kushiriki Simba imechukua Makombe 51 huku Yanga ikiwa na 42.
Lakini tuwe wakweli kidogo, kwanini Simba baada ya kuchukua ubingwa msimu uliopita wenzetu wameamua kujiita Mabingwa wa kihistoria?
Hivi Tanzania na nchi zote za Afrika Mashariki na kati ipi kubwa ya Simba na Yanga?
Simba ni Bingwa wa kihistoria wa ukanda huu wa Afrika, mbona sisi hatujiiti Mabingwa wa kihistoria wa zaid ya nchi 11?
Yaani sisi ni Mabingwa wa Mabingwa wa kihistoria. Haya njoeni na FACTS na mapovu.
Hivi mshawahi kusikia Manchester United au Mufurila Wonderes ya Zambia wakijiita Mabingwa wa kihistoria? BINGWA NI MMOJA TU. HAKUNA WA KIHISTORIA WALA JIOGRAFIA
Na Haji Manara (Ofisa Habari wa klabu ya Simba)








Hahahaa....hapo Manara Umenena.nawashangaa Yanga kujiita mabingwa wa kihostoria... sijui Bayern Munich wajiite mabingwa wa nini?
ReplyDeleteMabingwa wa kihistoria wapo tu miaka nenda miaka rudi. Brazil na world cup, Real madrid na uefa champions league etc. So kwa yanga ni sahihi wao kujiita hivo...
ReplyDeleteKwa hiyo Simba ni mabingwa wa kihistoria wa Afrika Mashariki na Kati na sio wa nchi moja tu.Au mantiki hiyo haifuatwi hapa?Jina hilo limezuliwa baada ya kupokwa ubingwa wa Tanzania.
ReplyDeleteHapa Simba Atakuwa Bingwa wa vikombe wakati yanga akibaki kuwa wa historia
ReplyDeleteWakosaji wote huwa wanajifariji.Yanga kama Manchester United wamebakia kusema ohh sisi wa historia.
ReplyDelete