September 7, 2018


Na George Mganga

Kocha Msaidizi wa klabu ya Simba, Mrundi, Masoud Djuma, ameibuka na kupuuzia taarifa zilizotoka hivi karibuni zikieleza kuwa ataondoka ndani ya timu hiyo muda wowote.

Djuma ameamua kufunguka baada ya taarifa hizi kuendelea kushika kasi kwenye baadhi ya vyombo vya habari na mitandao mbalimbali ili kuweka wazi ukweli na kuzipunguzia makali.

Kocha huyo ameeleza kuwa yeye bado ni mwajiriwa wa Simba na bado ana mkataba na mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2017/18 na akisema kuondoka ni ndoto kwake.

Djuma amesema bado anafurahia kusalia Simba akieleza ataondoka pale ambapo mkataba wake ukifikia mwisho na si sasa kwa sababu bado anahitajika kuihudumia timu.

Awali ilielezwa kuwa Djuma angeweza kuondoka Msimbazi kutokana na kukosa maelewano baina yake na benchi la ufundi haswa Kocha Mkuu, Patrick Aussems.

1 COMMENTS:

  1. Siyo "awali ilielezwa", sema champion liliripoti,chanzo cha uzushi huu ni Wewe mwenyewe hivyo usiache kujitaja.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic