September 7, 2018


Uongozi wa klabu ya Singida United umesema upo kwenye mazungumzo na kipa wake, Peter Manyika ili aweze kurejea kikosini.

Manyika ameamua kujiengua ndani ya timu hiyo kutokana na kushindwa kulipwa stahiki zake ikiwemo fedha za usajili na mishahara ya miezi kadhaa.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa klabu hiyo, Festo Sanga, ameeleza kuwa bado wanahitaji zaidi huduma ya Manyika kwa sababu amekuwa msaada mzuri kwenye lango lao ili kukiimarisha kikosi.

Sanga anaamini Manyika watamrejesha kwa kufika naye pazuri kimazungumzo ambapo kwa sasa yupo jijini Dar es Salaam akijifua kwenye kituo cha baba yake mzazi ili kuendelea kulinda kiwango chake.

Kuondoka kwa Manyika ndani ya walima alizeti hao kumeanza kuipa taswira mbaya ambapo ukichana na kipa huyo inaelezwa kuna baadhi ya wachezaji wengine pia wanaidai klabu.

1 COMMENTS:

  1. ACHENI KUENDESHA MAMBO YA UTAWALA KIUJANJAUJANJA. MKURUGENZI JANA ULIKANUSHA NA KUSEMA MANYIKA HAWADAI CHOCHOTE SASA LEO KAULI GANI HAPA UNATOA? USHAURI WANGU MANYIKA DAI HAKI YAKO ULIPWE LAKINI USIRUDI TENA NYUMA. HIVI AZAM KWANINI WASIKUCHUKUE ILI UKUZE KIWANGO CHAKO UKIWA UMETULIA? ONGEA NA AZAM.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic