September 17, 2018


Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam, RC Paul Makonda amelipongeza Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar  kwa juhudi kubwa walizozifanya za kuimarisha ulinzi na usalama kwenye vituo vyote vya Uchaguzi Jimbo la Ukonga kuanzia jana asubuhi mpaka mshindi alipotangazwa.

Makonda ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Askari katika Kituo Kikuu cha Polisi DSM (central) muda mfupi baada ya Matokeo kutangazwa na kuwataka waendelee kuwa majasiri kwani kazi yao ni ngumu na inahitaji uvumilivu wa hali ya juu.

Kwa upande wake Kamanda wa Kanda Maalum ya DSM, Lazaro Mambosasa, amesema kuwa katika uchaguzi huo ambao Mwita Waitara |(CCM) ameibuka mshindi, kikosi chake hakijatumia silaha ya aina yoyote sio risasi wala Bomu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic