MBELGIJI WA SIMBA AWAUZA WATANO ULAYA
Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems, ameweka wazi kuwa yupo katika mipango ya kuwauza wachezaji wake watano wa kikosi cha kwanza kwa klabu mbalimbali za nchini Ubelgiji anapocheza Mtanzania, Mbwana Samatta.
Kwa mujibu wa Championi, Aussems amesema kuwa amekuwa akipokea simu nyingi kutoka kwa viongozi wa klabu mbalimbali zinazoshiriki ligi kuu ya nchini humo wakiulizia wachezaji wa hapa wanaofaa kwenye kucheza kwenye ligi ya nchi hiyo.
Aussems amesema dhumuni la kutaka kuwauza wachezaji nje ni kwa faida ya nchini na wala siyo kufanya kazi ya uwakala kwa kuwa haimuhusu.
“Hapa Simba kuna wachezaji watano ambao kama mambo yakienda sawa huenda wakaenda kucheza Ubelgiji kwa sababu zipo baadhi ya timu zinawafuatilia na nimekuwa nikipokea simu kila wakati, hii imechangiwa na ubora wa Samatta pale KRC Genk.
“Unajua mimi siyo wakala na siwezi kufanya kazi hiyo ila naongea na wakurugenzi wa timu ambao wamekuwa wakiniuliza juu ya wachezaji wa hapa, wataanza kuja kuwaangalia kuanzia mwezi ujao, siwezi kuwataja majina kwa kuwa nitajenga matabaka kati yao,” alisema Aussems.
Habari njema vijana waongeze bidii na kufuata maelekezo ya kocha wamesharahisishiwa safari. wanasema kwenye fungu ndipo kuengezwapo kwani Simba ni kutamu vile vile.
ReplyDelete