September 15, 2018


Na George Mganga

Wakati kukiwa na baadhi ya wanachama wa klabu ya Simba wanaoipinga katiba mpya iliyopitishwa mwaka huu kutumika kwenye uchaguzi mkuu, Shirikisho la Soka Tanzania limewajibu kuhusiana na katiba inayopaswa kufuatwa.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Revocatus Kuuli, amesema katiba pekee inayopaswa kutumika ni ile iliyosajiliwa na Msajili wa Vyama vya Michezo nchini.

Kuuli amelitolea ufafanuzi hilo baada ya kupata taarifa kuwa kuna baadhi ya wanachama wamefika kwenye makao makuu ya shirikisho hilo kupeleka malalamiko ya kuikataa katiba mpya iliyosajiliwa mwaka huu.

Akizungumza na Radio One kupitia Spoti Leo, Mwenyekiti huyo amesema katia pekee wanasimba wanayopaswa kuitumia n ile iliyopitishwa na klabu kisha kusajiliwa kwa kufuata taratibu zote ambazo ziliafikiwa na wanachama wake.

Wanachama hao baadhi wamekuwa wakiendeleza wimbo wa kuipinga katiba hiyo ilihali ilipitishwa na wanachama wa Simba katika mkutano mkuu uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam wakati wa kupitisha mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshwaji wa klabu.

Hata hivyo tayari Simba imeshaifanyia marekebisho katiba mpya iliyosajiliwa na Msajili Mkuu kutoka Serikalini, Ibrahim Mkwawa mwaka huu.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic