Suleiman ambaye aliwahi kutamba na kikosi hicho cha wekundu wa Msimbazi miaka ya nyuma, amesema kilicheza mpira wa kiufundi japo hakikuweza kutumia vema nafasi walizozipata.
Mchezai huyo wa zamani ameeleza kuwa Simba haikuwa na bahati na ilistahili kupata matokeo lakini wapinzani wao waliwazuia vilivyo haswa kwenye eneo la ulinzi.
Kitendo cha Mbao kukaza zaidi eneo la ulinzi kiliwapa Simba ugumu wa kufunga huku nafasi kadhaa alizozipata mchezaji, kiungo Shiza Kichuya ziliwagharimu zaidi Simba.
Suleimani anaami timu hiyo itafanya vizuri zaidi mbele ya safari akiamini bado mechi ni nyingi zilizosalia na huu ndiyo mwanzo wa ligi.
basi point 3 watachukua wao maana walicheza vizuri huu ndo umbumbumbu unaozungumzwa chenga twawala ila tumefungwa sijui bingwa anapatikana kwa pont nyingi au kwa kucheza vizuri
ReplyDelete