MO AFANYA KWELI SIMBA
Mwekezaji Mkuu wa Simba, Mohammed Dewji ‘MO’, jana usiku alitarajiwa kukutana na wachezaji na benchi la ufundi la timu hiyo ili kuwapa moyo kuelekea kwenye mchezo wao dhidi ya Yanga.
Simba inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Yanga kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu msimu huu baina ya timu hizo.
Mo ambaye ni msaada mkubwa ndani ya Simba, alitarajiwa kukutana na wachezaji na benchi la ufundi ambao wapo kambini katika Hoteli ya Sea Scape jijini Dar.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya klabu hiyo, kimeliambia Championi Jumamosi kuwa, mwekezaji huyo alitarajiwa kwenda kambini kuwatia moyo wachezaji na benchi zima la ufundi la timu hiyo kabla ya mchezo wa kesho dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga.
“Taarifa tulizonazo hapa ni kuwa leo (jana) usiku Mo atakuja kuzungumza na wachezaji jambo ambalo ameliahidi tangu juzi (Jumatano) na kama hatakuja leo (jana) basi ni lazima aje kesho (leo) kuwapa moyo ili waingie uwanjani wakiwa na hali ya kujiamini zaidi.
“Najua hataishia kutoa maneno tu, lazima kutakuwa na fungu la pesa atakalokuwa ameliandaa kama sehemu ya hamasa zake na jinsi ninavyofahamu kuna uwezekano wa kutoa zaidi ya shilingi milioni 10,” kilisema chanzo hicho.
0 COMMENTS:
Post a Comment