September 23, 2018


Baada ya kumtwanga bondia kutoka England, Samm Eggington, Mwekezaji wa klabu ya Simba amempa ufadhili Bondia Mtanzania, Hassan Mwakinyo kuelekea pambano lake dhidi ya Wanik Awdijan.

Mo ameamua kuwekeza nguvu zake kifedha kwa Mwakinyo ili kumtengenezea mazngira ya kuzidi kufanya vizuri ambapo atakuwa anachuana na Awdijan kutoka Ujerumani Oktoba 20 2018.

Taarifa hizo zimekuja mara baada ya Mwakinyo kukosa watu wa kumuwezesha kupata maandalizi ya kutosha na sasa bila shaka ndoto yake imezidi kunawili kutokana na kupata nguvu kwa Bilionea huyo kijana ndani ya Afrika.

Mwakinyo atakuwa na kibarua hicho ambacho kitafanyika huko Ujerumani tayari kuweka rekodi nyingine itayoweza kuipeperusha vema bendera ya Tanzania.

1 COMMENTS:

  1. Kama ni kweli yasemwayo basi Hongera sana Mo kwa kuonesha uzalendo na uzendo na upendo wa dhati katika hili.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic