MOTO WA YANGA NI BALAA HUKO MOROGORO, ZAHERA ADILI NA STRAIKA MMOJA
Na George Mganga
Kikosi cha Yanga jana kimeendelea kujifua na mazoezi mahususi ya kuandaa dozi maalum dhidi ya Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaofanyika Septemba 30 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika mazoezi hayo Kocha Mkongomani, Mwinyi Zahera, alionekana kuwapa mazoezi ya pumzi wachezaji wake ikiwemo kukata upepo ili kuhakikisha wanaihimili Simba vilivyo.
Zahera amezidi kukifua vema kikosi chake ambacho kimeweka kambi maalum mjini Morogoro, sehemu ambayo utulivu wa aina yake ili kuwaandaa vema wachezaji kwa mechi hiyo kubwa.
Unaambiwa Zahera amewaongoza wachezaji kwa kutengeneza muunganiko mzuri haswa sehemu ya kiungo pamoja na safu ya ushambuliaji, huku akimpa nafasi Tambwe ya kuhakikisha anafanya maangamizi siku hiyo.
Kocha Zahera anaamini Tambwe atafanya vizuri baada ya kuisaidia Yanga kuibuka na ushindi wa mbao 2-0 dhidi ya Singida United kwenye mchezo wa mwisho wa ligi uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar.
Noma
ReplyDeleteKiukweli kabisa huwezi tafuta au pata pumzi kwa siku 3 au 5...utaniambia kama siyo kuona wachezaji wachovu wote
ReplyDeletelabda kawajaza kwa pampu
ReplyDelete