September 28, 2018


Na George Mganga

Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania inakukatana leo kwa ajili ya kujadili masuala kadhaa ikiwemo lile la sakata la Wakili Revocatus Kuuli na Katibu wa TFF, Wilfred Kidao.

kwa mujibu wa Kuuli ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati hiyo, amesema wanakutana leo kunako makamo makuu ya Shirikisho hilo kuweka sawa mambo kadhaa ili kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa.

Kikao hicho kimekuja mara baada ya Kuuli kuelezwa kuandikiwa barua na Katibu Mkuu wa TFF, Kidao barua ya kueleza kwanini ameusimamisha mchakato wa uchaguzi Simba pia ikimtaka aeleze ametoa wapi mamlaka hayo.

Baada ya kusambaa kwa barua hiyo, Kuuli alikuja juu na kusema Kidao hawezi kuiingilia kamati huru ambayo hahusiki nayo na akisisitiza kuwa maamuzi yake yalikuwa sahihi.

Sakati hilo sasa limechukua taswira mpya ambapo Kuuli atakaa na kamati hiyo leo kujadili kwa kina sintofahamu hiyo iliyosababishwa na mchakato wa uchaguzi wa Simba ambao mpaka sasa unaendelea kama kawaida.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic