September 24, 2018


Mbunge wa Ukerewe, Joseph Mkundi ambaye alitoa tahadhari kwa serikali na kuikumbusha kukarabati kivuko cha MV Nyerere kabla hajisababisha maafa, amefunguka muda mfupi baada ya mazishi ya marehemu wa ajali hiyo kisiwani Ukara.

Mkundi ameitaka Serikali kuweka kikosi maalum cha uokoaji kwa Kanda ya Ziwa kwani eneo hilo lina vyombo vingi vya majini, na ajali ni nyingi, lakini ppia wakazi wa eneo hilo wanategemea zaidi usafiri wa maji ili kurahisisha shughuli zao kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Mbunge huyo ameongeza kuwa siku ya tukio vyombo kikosi cha uokoaji kilichelewa, kwani ajali ilitokea saa 8, lakini waokoaji walifika saa 11 hivyo tayari watu wengi walikuwa wameshapoteza maisha, lakini wangewahi, wangeokoa watu wengi wakiwa hai.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic