September 3, 2018


Mwananachama maarufu wa Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali ametamba kwamba kiungo wa timu hiyo, Feisal Salum ‘Fei Toto’ ni bonge la mchezaji na hakuna mfano wake.

Akilimali ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Yanga, amemfananisha mchezaji huyo na staa wa zamani wa Zanzibar, Abdul Matiham ambaye alikuwa na chenga za maudhi sana miaka ya nyuma.

Fei Toto ambaye amesajiliwa na Yanga msimu huu akitokea JKU ya Zanzibar, ameonyesha kiwango katika timu hiyo ikiwa ni pamoja na kuwa tegemeo kwenye kikosi cha kwanza huku viongozi wakimuonya akae mbali na baadhi ya mashabiki wa kike ambao wanamnyemelea.

Akilimali alisema; “Fei Toto ni mchezaji mzuri sana yaani ananikumbusha mbali sana enzi za mchezaji wa Zanzibar, Abdul Matiham ambaye alikuwa akipiga chenga sana na alikuwa akifanya vizuri enzi hizo.

“Nina imani kuwa atafanya vyema sana mbele ya safari, ameonekana kuanza vizuri sana kiwango chake ni kizuri hivyo namsihi aendelee kujituma.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic