September 28, 2018


Staa wa kikapu katika Ligi ya NBA, LeBron James amesema uamuzi wake wa kuhamia Los Angeles Lakers umechagizwa na sababu za mchezo huo na siyo kuhusu masuala ya filamu za Hollywood.

Mkali huyo ambaye ni mshindi mara nne wa Tuzo ya Mchezaji Mwenye Thamani NBA (NBA Most Valuable Player) alitua Lakers, Julai mwaka huu kwa dili la miaka minne ambalo lina thamani ya dola 154m, amekuwa gumzo huku baadhi ya mashabiki wakiamini sababu za kutua hapo ni kuhusu kuwa karibu na Hollywood.

James, 33, amehusika katika filamu na tamthilia kadhaa, alipoulizwa juu ya hilo katika mkutano wake na waandishi alisema: “Uamuzi wangu ulitokana na familia na Lakers wenyewe, mimi ni mchezaji wa kikapu, ni sehemu ya biashara yangu, hayo masuala mengine yamekuwa yakitokea hata kabla ya mimi kuja hapa.” 

Nje ya uwanja kampuni yake ya, SpringHill Entertainment imejihusisha na miradi kadhaa ikiwemo filamu.

Lakers inaweza kuwa bingwa wa NBA? James ametokea katika fainali nane akiwa kwenye timu zake zilizopita za Cleveland Cavaliers na Miami Heat, lakini mara ya mwisho kwa Lakers kufika fainali ilikuwa mwaka 2010. 

Kuhusu hilo, James amewaambia mashabiki kuwa wasitegemee mambo makubwa ndani ya muda mfupi ikiwemo kuwania ubingwa dhidi ya Golden State Warriors ambao ni mabingwa watetezi.

“Tuna safari ndefu kufikia levo ya kuwania ubingwa, muhimu ni kuangalia kwanza ubora wetu wa sasa, tucheze kama timu na kisha ndiyo tuwafikirie Golden State,” anasema James. 

Lakers kurudisha heshima J a m e s ana mzigo mkubwa wa kurudisha heshima ya timu hiyo iliyowahi kuwa na mastaa wengi k a m a K o b e Bryant, Magic Johnson , Kareem AbdulJabbar na Shaquille O’Neal. “Tunajua timu hii imekuwa ya kihistoria, ni timu ya ubingwa, ni jambo zuri kuwa ndani ya jezi hii,” anasema James.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic