September 28, 2018


Juventus na AC Milan zinapania kumsajili kiungo wa kati wa Arsenal Aaron Ramsey. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 huenda akaondoka klabu hiyo msimu huu wa joto.

Arsenal iko tayari kumuuza Ramsey mwezi Januari isije ikaambulie patupu kwa kutoa bila malipo.(Mirror)

Barcelona inamfuatilia kiongo wa kati wa Manchester United na mfaransa Paul Pogba, 25, licha ya changamoto zinazomkabili katika klabu hiyo. (Independent)

Kuna hofu mvutano kati ya mkufunzi wa Man Utd Jose Mourinho huenda umewaathiri wachezaji wengine.

Antony Martial na Andreas Pereira wanadaiwa kushangazwa na mienendo ya hivi karibuni ya meneja wao Mourinho. (Mail)


Paul Pogba na Jose Mourinho walionekana wakirushiana cheche za maneno wakati wa mazoezi siku ya juma tano.

Baadhi ya wachezaji wa United wamekasirishwa na hatua ya Mourinho kuwakosoa hadharani walinzi Eric Bailly na Phil Jones baada ya kushindwa na Derby katika kombe la Carabao Jumanne hii. (Sun)

Ajenti wa Pogba, Mino Raiola, anatarajiwa kukutana na maafisa wa United mwezi Novemba kujadili hatima ya siku zijazo ya kiungo huyo wa kati. (Guardian)

Mourinho amemkemea mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, mwenye umri wa miaka 20, kwa kushindwa kupumzika vya kutosha baada ya ushindi wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Young Boys wiki iliyopita. (Mail)

Kiongo wa kati wa Chelsea Cesc Fabregas ,anaamini itakuwa vigumu kwa klabu hiyo kuendelea kumkwamilia Eden Hazard.

Mchezaji huyo raia wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 27 alitaka kuondoka Stamford Bridge mwezi Julai lakini Chelsea ilisema haiko tayari kumuuza. (Evening Standard)

Kiungo mwenzake katika kilabu hiyo Ross Barkley amesema kwa sasa Hazard ni bora kuliko Lionel Messi wa Barcelona na Cristiano Ronaldo wa Juventus Cristiano Ronaldo. (Guardian)


AC Milan imeonyesha nia ya kumnunua Fabregas, 31, na imesema kuwa iko tayari kujishindia mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania mwezi Januari mwakani (Mundo Deportivo - kwa kihispania)

Kutoka BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic