September 1, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa Ofisa Habari wake, Haji Manara, umesema sakata la wachezaji wake na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeshamalizika hivyo amewaomba watanzania wote waisapoti timu hiyo.

Kauli ya Manara imekuja kufuatia Kocha Mkuu wa Stars, Emmanuel Amunike kuwaondoa wachezaji 6 wa Simba baada ya kuchelewa kuripoti kambini, lakini baadaye alikutana na kuzungumza nao kisha kuwasamehe.

Kutokana na kitendo cha Amunike kuwasamehe wachezaji hao, Manara amewaomba watanzania wote wakaipe sapoti timu ya taifa itakapocheza na Uganda hasusani waliopo kanda ya ziwa.

Ofisa huyo amesema hakuna haja ya kuitenga timu kutokana na na baadhi ya mashabiki wa Simba kuibuka na kueleza wataisaliti kwa kuipa sapoti Uganda baada ya kupatwa na hasira sababu za wachezaji wao kuondolewa.

Stars itacheza na Uganda Septemba 8 huko Kampala ukiwa ni mchezo wa kufuzu kuelekea fainali za AFCON 2019.

4 COMMENTS:

  1. ULIKUWA UAMUZI MBAYA USIOLETA UMOJA WALA TIJA KWA TIMU YETU. TUSIFANYE MAAMUZI KWA PUPA NA JAZBA MWISHO WA YOTE TUNAIKOSESHA HESHIMA TANZANIA. WACHEZAJI WOTE NI WATOTO WA TANZANIA.

    ReplyDelete
  2. IT WAS A BAD DECISION MADE BY THE NATIONAL COACH

    ReplyDelete
  3. Tatizo liliopo ni nidhamu na ni masulia ya nidhamu yapo kwa TFF badala ya kutimua wachezaji wajenge nidhamu na bila ya nidhamu, fujo ndio inayotawala na tutabakia hihivi bila ya Mandeleo yoyote. Nyumba bila ya msingi madhubuti haidumu. Ili kujenga nidhamu hapana budi TFF kujenga sheria ya kuwaweka sawa wachezaji wakorofi katika timu. Vilabu bila nidhamu na maendeleio manaake timu ya taifa bila ya nidhamu na maendeleo. TFF itunge sheria kuwadhibiti wachezaji wakorofi katika vilabu, sheria ambayo lazima itekekelezwe na viongozi au nao waadhibiwe. Mchezaji leo anachelewa mazoezini, kagoma, kawacha kuhudhuria na mengi mengineo. Itungwe sheria ya kuwaadhibiti wakorofi hao, kwa kuwaziwia kucheza, kuwakata posho na mishahara pamoja hata kuzuwiwa wasicheze mpira kwa muda wa mwaka au zaidi. Kuyafanya hayo ndipo tutapofanikiwa kudhibiti nidhamu katika vilabu na timu za Taifa na hakuna jenginelo. Tusifike kwa hekima na ubora wa timu na wachezaji wake na sio kutimuwa kuzidi kukoroga mambo na Mungu atatusaidia baada nasi kujisaidia

    ReplyDelete
  4. Yes, not only bad, but also very detructive. Reciprocity is the only way to instructive solution. Thank God, the coach responded to public cries and saved the would be sad situation. TFF also deserves thanks for cooling down the atmosphere

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic