September 1, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza michango ya fedha iliyoingia klabuni kupitia michango ya wanachama na mashabiki wake kwa mwezi wa 8.

Michango hiyo ambayo imeanza kuchangwa kuanzia Agosti 2 mpaka kufikia jana Agosti 31, imefikia kiasi cha shilingi za kitanzania milioni 29,316,092.


Licha ya kukusanya kiasi hicho cha fedha, uongozi Yanga umezidi kuwaomba wapenzi, mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kuendelea kujitoa.

Hatua hiyo imekuja kutokana na klabu kupitia kipindi cha mpito haswa tangu aliyekuwa Mwenyekiti wao, Yusuf Manji kutangaza kujiuzulu nafasi hiyo.

Kituo cha Azam TV kimeonesha nia ya kuipa sapoti Yanga kwa kuisaidia kutoa PROMO ya kuwatangazia watazamaji wake namna ya kuichangia klabu hiyo kupitia mitandao ya Tigo Pesa, Airtel Money na M-Pesa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic